Dereva wa Basi la Mwendokasi (BRT) atawajibika kuendesha basi la mwendokasi kwa
usalama, umakini na weledi, kwa kuzingatia ratiba, njia na vituo vilivyopangwa.
Pia atahakikisha usalama wa abiria, kufanya ukaguzi wa basi, kuzingatia sheria
za barabarani na taratibu za BRT, pamoja na kutoa huduma bora kwa abiria.
Muombaji
mwenye Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne (IV) NA Kidato cha Sita (VI), awe na Leseni
ya Udereva Daraja C Plain iliyohakikiwa na Jeshi la Polisi, Cheti cha PSV
kutoka VETA au NIT, Cheti cha BRT kutoka NIT na awe na uzoefu wa kazi wa
angalau miaka 3 katika udereva wa magari ya abiria au mabasi.
Ø Kuendesha
basi la mwendokasi kwa usalama, umakini na kuzingatia ratiba na vituo
vilivyopangwa.
Ø Kuhakikisha
usalama wa abiria, watumiaji wengine wa barabara na mali wakati wote wa safari.
Ø Kufanya
ukaguzi wa basi kabla na baada ya safari ili kuhakikisha liko katika hali nzuri
na salama kwa matumizi.
Ø Kuripoti
mara moja hitilafu za kiufundi, ajali, matukio au changamoto nyingine
zinazojitokeza wakati wa safari kwa msimamizi husika.
Ø Kuhakikisha
basi linatunzwa, linakuwa safi na katika hali nzuri wakati wote wa matumizi.
Ø Kuzingatia
sheria na kanuni za usalama barabarani, taratibu za BRT na miongozo ya kampuni.
Ø Kutoa
huduma bora kwa abiria kwa heshima, staha na weledi.
Ø Kufuatilia
muda wa mwisho wa uhalali wa nyaraka za dereva kutoa taarifa kwa wakati kabla
ya nyaraka hizo kuisha muda wake.
Ø Kuhifadhi
na kuwasilisha kwa usahihi taarifa za safari, matumizi ya nishati ya gesi na
taarifa nyingine muhimu za uendeshaji wa basi.
Ø Kutoa
msaada na kufuata taratibu za usalama wakati wa dharura, ajali au matukio
mengine yasiyotarajiwa.
Ø Kuwa makini
zaidi katika maeneo yenye vivuko vya waenda kwa miguu (zebra), vituo vya BRT na
maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu.
Ø Kushirikiana na wasimamizi, waendeshaji wenzake na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha huduma ya usafiri inatolewa kwa ufanisi na kwa usalama.
GRADE 4